Tuesday, 6 March 2012

taarifa ya MAT ya kuendelea na mgomo

THE MEDICAL ASSOCIATION OF TANZANIA

MSIMAMO JUU YA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI


Kama tulivyotoa taarifa kwenye kikao cha Madaktari cha Machi 3, 2012 ni kwamba makubaliano yaliyofikiwa na hatimaye kutiwa saini kati ya Serikali na Madaktari tarehe 2.3.2012 ni kuwa, ili meza ya mazungumzo ya kujadili madai ya Madaktari iweze kuendelea na hatua ya pili, ni lazima Waziri wa Afya (Dkt. Mponda) na Naibu wake (Dkt. Lucy Nkya) ama wajiuzulu au wawajibishwe kama ilivyokuwa imeahidiwa na Mh. Waziri Mkuu Februari 9, 2012 alipofanya kikao na Watumishi wa Afya pale Hospitali ya Taifa, Muhimbili.

Aidha, kulingana na makubaliano haya, kikwazo kikubwa cha kutokuendelea kwa majadiliano ya madai ya Madaktari (Uboreshaji wa huduma wapatazo wagonjwa, mazingira mazuri ya kufanyia kazi na maslahi kwa ujumla wake) ni kuendelea kuwepo kwa Dkt. Mponda na Dkt. Lucy Nkya kweney nafasi zao za Kiuongozi.

Hivyo basi, kwenye huo mkutano wa Machi 3, 2012, baada ya majadiliano na tafakari za kina, ilikubaliwa kwa pamoja kuwa watu hawa wawili wanatakiwa kuachia ngazi mara moja ili haki za wagonjwa na madai ya Madaktari yaweze kujadiliwa na kutekelezwa.

Hivyo basi, iliamuliwa kuwa kama mpaka siku ya Jumatano, Machi 7, 2012 bado akina Dkt. Mponda na Dkt. Lucy Nkya watakuwa bado wapo madarakani, wataanza mgomo rasmi kushinikiza ama wajiuzulu au wawajibishwe ili taratibu nyingine ziweze kuanza.

Kama ilivyo taratibu ya chama kutoa taarifa kwa wanachama kote nchini, ifahamike kwamba mkutano uliamua kuwa Madaktari wote kuwa kuanzia Jumatano (Machi 7, 2012) watasitisha kutoa huduma zote za afya katika hospitali zote nchini mpaka hapo Serikali itakapoonesha utayari kwa kutimiza ahadi yake ya kuwawajibisha watajwa hapo juu ili hatua nyingine za utekelezaji wa madai ya Madaktari kwa manufaa ya Taifa yawze kuanza kushughulikiwa.

Ifahamike kwamba chama kinasikitishwa sana na kitendo cha Viongozi Waandamizi wa Wizara ya Afya ambao wanajua umuhimu wa kuwajibika kwa mara nyingine tena wanafanya Madaktari waendelee kutetea haki za Watanzania katika njia ngumu na kwa nia ya kufanikisha malengo haya kwa faida ya Watanzania wote.

IMETOLEWA NA OFISI YA M.A.T MAKAO MAKUU.

DR. NAMALA MKOPI
RAIS WA MAT
05/03/2012

All correspondence to: the Hon. Secretary General, MAT.

Tel. +255 22 2151835
Fax: +255 22 2153514
e-mail: info@mat-tz.org
website: www.mat-tz.org

Muhimbili University Complex,
Ruvu Block – Ground Floor,
P.O. Box 701,
Dar es Salaam,
Tanzania.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/03/msimamo-wa-mat-juu-ya-utekelezaji-wa-madai-ya-madaktari.html?utm_source=feedburner&utm_medium=feed&utm_campaign=Feed%3A+wavuti+%28Wavuti%29&utm_content=FaceBook#ixzz1oSIDtH8h

No comments:

Post a Comment